Propellerads

Simba yawapa taadhari wapinzani


Image result for picha za Daniel Agyei

SIMBA imejibu mapigo ya mahasimu wao, Yanga, baada ya jana mchana kumleta kipa wa timu ya taifa ya Ghana, Daniel Agyei kuja kusaini kuichezea timu hiyo kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu, zikiwa zimepita saa 24 tangu wapinzani wao, Yanga kumleta nchini Justine Zullu raia wa Zambia.
Image result for picha za Daniel Agyei
Agyei, ambaye ni kipa wa zamani wa timu ya taifa ya Ghana ya umri wa chini ya miaka 20, aliwasili Dar es Salaam jana mchana na kupokewa na aliyekuwa Meneja wa timu hiyo, Abbasi Ally na kuelekea mapumziko na leo Alhamisi anatarajia kukutana na viongozi wa juu wa timu hiyo ili kumalizia mazungumzo yao na kusaini mkataba wa kuwatumikia Wanamsimbazi.
Akizungumza na gazeti hili msemaji wa Simba, Haji Manara, alisema ujio wa kipa huyo ni ishara ya kuelekea kuwa mabingwa wa Tanzania Bara, msimu huu kama walivyokusudia mwanzoni mwa msimu.
“Tumesema atakuja na leo (jana), amewasili, kilichobaki kwetu ni ubingwa kwa sababu tayari tumemaliza ugonjwa mkubwa ambao ulikuwa ukitutia hofu kwenye nzunguko wa kwanza,”alisema Manara.
Image result for picha za Daniel Agyei
Mchezaji huyo ameletwa nchini kutokana na repoti ya kocha wao Joseph Omog, raia wa Cameroon, kuuagiza uongozi kutafuta kipa mwingine ambaye atampa chalenji Vicenti Agban ambaye amedaka peke yake mechi zote za mzunguko wa kwanza.
Alisema kutua kwa Agyei haimaanishi kuwa watamtupia virago Agban, bali wataendelea kuwa naye pamoja na kinda Manyika Peter, ili kuongeza ushindani wa kuwania nafasi ya kucheza wenyewe kwa wenyewe.
“Hao wote ni makipa wetu na bado tunawahitaji ndiyo maana tutaendelea kubaki nao kwenye timu kwa ajili ya kuongeza ushindani kwa kipa namba moja ambaye atachaguliwa na benchi la ufundi linaloongozwa na kocha Omog,”alisema Manara.
Agyei anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili na mabingwa hao wa zamani wa Tanzania na uwezekano wa kipa huyo kushindwana na Simba ni mdogo, kwani tayari ameutaka uongozi wake wasimjumuishe kwenye mipango yao ya msimu ujao.

IMEANDIKWA NA MOHAMED AKIDA
Previous
Next Post »