KILIO cha uhaba wa chakula katika mikoa mbalimbali hapa nchini, kutokana na ukame kimelifikia kanisa Katoliki na sasa limeagiza maombi mazito yaanze ili kunusuru maisha ya wananchi, anaandika mwandishi wetu.
Agizo hilo la kanisa Katoliki linakuja katika kipindi ambacho serikali ya Tanzania kupitia Rais John Magufuli imeapa kutopeleka chakula kwa wananchi wanaoripotiwa kukumbwa na janga la njaa.
Barua ya Tarcisius Ngalalekumtwa, mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) kwenda kwa Wahashamu Mababa Maaskofu imesema, “Ziadhimishwe Misa za kuomba mvua. Kuwepo na hija, mfungo na mikesha ya maombi maalum.”
Rais Magufuli amenukuliwa katika ziara zake za kiserikali mkoani Kagera, Simiyu na Shinyanga akisema kuwa, “Serikali yangu haitatoa chakula cha msaada. Haiwezekani serikali itoe elimu bure, itoe dawa, maji na barabara lakini pia itoe chakula bure. Serikali haina shamba.”
Rais Magufuli pia amesema, “Rais ndiye mwenye uwezo wa kujua kama kuna njaa au la.”
Katika barua ya mwenyekiti wa TEC amesema anaomba kasi ya sala iongezeke kote nchini.
Katika barua ya mwenyekiti wa TEC amesema anaomba kasi ya sala iongezeke kote nchini.
“Mungu aliyewatunza wana wa Israel walipokuwa safarini kuelekea nchi ya ahadi kwa miaka 40 atuangalie kwa wema, huruma na upole. Tuombe Baraka juu ya kazi zetu za kilimo, tukayapate mazao ya nchi,” amesema.
ConversionConversion EmoticonEmoticon