Propellerads

Rick Ross azidi kutetereka kiuchumi


Image result for picture of rick ross sold house

Hali ya kiuchumi ya rapper Rick Ross inazidi kuwa mbaya – baada ya kukosa mteja wa kununua nyumba yake ya mjini Florida sasa ametangaza kuiuza kwa bei ya hasara.
Imeripotiwa kuwa rapper huyo ametangaza kuuza nyumba hiyo kwa kiasi cha dola milioni 1.3 wakati hapo mwanzo alitangaza kuiuza kwa kiasi cha dola milioni 1.5.

Image result for picture of rick ross sold house


Nyumba hiyo yenye vyumba 6 vya kulala, mabafu 5, jiko kubwa, studio mbili za kurekodi aliinunua mwaka 2008 kwa kiasi cha dola milioni 1.25 na itakuwa ni nyumba yake ya pili kuiuza kwa mwaka huu baada ya ile ya kwanza aliyoiuza kwa kiasi cha dola milioni 6.
Previous
Next Post »