Joh Makini
ameweka wazi kuwa hafanyi muziki mzuri kwa
kuangalia kuja kuwa nominated kwenye
tuzo flani.
Rapa huyo
kutoka kwenye kundi la Weusi, amezungumza hayo baada ya kuwepo kwa maswali
mengi kuwa mbona hajatajwa kuwania Tuzo za kimataifa zikiwemo MTV kwa mwaka huu
ilihali akiwa na ngoma kali kama Don’t Bother aliyo mshirikisha AKA
kutoka Afrika kusini.
Lakini pia
Joh ameweka wazi kuwa juhudi zake sio muziki wa Afrika Mashariki tu, Ni muziki
wa Dunia na ana amini amefanya vitu vichache sana japokuwa watu wanaona
amefanya vitu vikubwa huku yeye akipanga kufanya muziki mzuri zaidi na mkubwa.
Tutarajie
makubwa mengi kutoka kwa Rapa Joh Makini kwenye muziki wake.
This is dummy text. It is not meant to be read. Accordingly, it is difficult to figure out when to end it. But then, this is dummy text. It is not meant to be read. Period.
ConversionConversion EmoticonEmoticon