Dili la Jay Z la kutaka kununua haki
miliki ya nyimbo za marehemu Prince aliyefariki mwezi April, mwaka huu
limekataliwa.
Chanzo kutoka kwenye familia ya
marehemu Prince kimeuambia mtandao wa TMZ kuwa familia hiyo haina mpango na
dili hilo kwa kuwa bosi huyo wa mtandao wa Tidal [Jay Z] alishawahi
kujimilikisha albamu 15 za prince bila ya kibali.
Mwezi uliopita Jay Z aliweka wazi
juu ya kununua haki miliki za nyimbo za Prince ambazo bado hazijatoka kwa
kulipa kiasi cha dola milioni 40 baada ya kufanya mazungumzo na ndugu wa
Prince, Tyka.
ConversionConversion EmoticonEmoticon