Baada ya kuigiza filamu takriban
200, hatimaye Jackie Chan 62, ametunukiwa tuzo ya heshima ya Oscar.
Muigizaji huyo wa China alipewa tuzo
hiyo Jumamosi kwenye tuzo za Governors.
Jackie Chan aliwaambia watu kuwa
kuna wakati alikuwa akiangalia tuzo hizo na wazazi wake ambapo baba yake
alimuuliza iweje hajawahi kushinda Oscar licha ya kuwa na filamu kibao.
Alitambulishwa na staa mwenzake wa
filamu ya “Rush Hour” Chris Tucker, muigizaji Michelle Yeoh na Tom Hanks,
ambaye alimuelezea kama “Jackie ‘Chantastic’ Chan.”
Hanks alisema kuwa ni jambo zuri
kutambua kazi za Chan kwa sababu filamu za martial arts na action comedy,
zimekuwa zikitengwa kwenye tuzo.
Muigizaji mkongwe, Arnold
Schwarzenegger amempongeza Chan kwa tuzo hiyo.
Kwenye picha hiyo juu aliyoiweka
Instagram, Schwarzenegger ameandika: Congratulations to my great friend
Jackie Chan on his fantastic honor – after 200 movies, you certainly deserve
this Oscar. You always inspire.
ConversionConversion EmoticonEmoticon