Baraza la Sanaa Taifa (BASATA)
ambalo ni walezi wa wasanii pamoja na shughuli za sanaa nchini, limekiri kusikia
tetesi za bifu inayoendelea kati ya mastaa wawili wa muziki nchini, Alikiba na
Diamond.
Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Taifa
(BASATA), Godfrey Mngereza amesema
amesikia kuna bifu kati ya Diamond na Alikiba lakini hawajapokea taarifa rasmi yenye kuonyesha mmoja kati yao akilalamika kuhusu mwenzie.
Aliongeza, “Lakini tukikutana na wao
wenyewe wapo safi, kwa hiyo wanaosababisha hivyo ni mashabiki kwa sababu hata
wachezaji wa Simba na Yanga wale ni wachezaji wapo kwenye tasnia moja, ni
marafiki wanakaa pamoja, wanakula pamoja ni kama wanamichezo wa ngumi, wewe
ukiwa nje unaangalia wao wanapigana kweli utasema kuwa wanavita lakini si kweli kwakua ule ni mchezo.
Kwahiyo mimi
hii naona ni ushabiki wa mashabiki ambapo kimsingi huwezi kuwazua. Pia ni kwa
sababu hakuna aliyelalamika, kimsingi sisi ni walezi wa wasanii mmoja angelalamika
sisi tungeuwita upande mwingine,”
ConversionConversion EmoticonEmoticon