Eddy Kenzo kutoka Uganga ni
msanii anaye fanya vizuri kimuziki
Afrika Mashariki na pia Afrika kiujumla ni mmoja wa wasanii wa Uganda waliofanikiwa
sana kwa sasa.
Akihojiwa na chombo kimoja cha haari
alisema; hadi sasa ana nyumba tatu huku moja ya kifahari ikiwa Seguku, Kampala.
“One is for my studio where I work,
my work place, another one in my village Masaka, then that one (Seguku),” amesema
Eddy.
Anasema kwa upande wa magari anayo
manne.
Akizungumzia muziki wa Uganda, Eddy
amesema soko la muziki la nchi yao ni kubwa na wasanii wengi ni matajiri kwa
fedha za ndani. Aliwataja wasanii wengine wa nchini Uganda wenye utajiri mkubwa
kama Bobi Wine, Chameleon na Bebe Cool amabaye kwa sasa anatamba na kibao
kiitwacho “Kaburenge”. Aliongeza kwa
kusema tasnia ya Muziki nchini humo ni
kubwa sana na wanamuziki hufanya show Jumatatu hadi Jumapili na kujaza kumbi, wanapata pesa nyingi hata bila kufanya show nje ya nchi.
Kwa upande mwingine Eddy Kenzo
anatarajia kufanya collabo na msanii wa Tanzania lakini hakutaka kumtaja.
Anasema album yake mpya itaitwa Biology
na itakuwa na nyimbo 20.
ConversionConversion EmoticonEmoticon