Propellerads

Dr Mwele Malechela asema asema"safari itasonga kwa msaada wa Mungu"


Image result for pictures of Dr Mwele Malecela

BAADA ya kutenguliwa kwake na Rais Dkt. John Magufuli, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu, NIMR, Dr Mwele Malechela, ametoa kauli yake jana Ijumaa.
Kutenguliwa kwa Dkt. Mwele kumekuja siku moja tu baada ya kuzungumza na waandishi na kudai kuwepo kwa virusi vya Zika nchini. Alisema kati ya watu 533 waliopimwa wakati wa utafiti walioufanya, asilimia 15.6 waligunduliwa kuwa na virusi hivyo. Taarifa yake, ilikuja kukanushwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.
Akijibu tweet iliyosema, ” Pole sana @mwelentuli safari yako na isonge mbele Dada,” Dr Mwele amesema, “Ahsante na itasonga kwa msaada wa Mungu.”
Tweet nyingine alijibu: Ahsante Mathew. Nilipewa dhamana nimetumikia ninamshukuru Mungu kwa nafasi ya kutumikia WaTanzania kupitia utafiti.”

Image result for pictures of Dr Mwele Malecela
dkt-mwele
Ahsante Mathew. Nilipewa dhamana nimetumikia ninamshukuru Mungu kwa nafasi ya kutumikia WaTanzania kupitia utafiti https://twitter.com/mathewmndeme/status/809857623663198212 

Previous
Next Post »