HATIMAYE staa wa muda wote katika muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ a.k.a Jide leo amekiri bila kupepesa maneno kuwa yupo katika penzi zito na mwanamuziki mwenzake raia wa Nigeria aitwaye Chris maarufu kama Spicy a.k.a Rasta.
Jide ameyafunguka hayo wakati akifanya Exclusive Interview na Global TV Online kwenye studio zake zilizopo ndani ya Ofisi za Global Publishers Ltd eneo la Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam.
Mbali na kuwa katika mahaba na Rasta, Jide amefunguka kuwa tayari wana project ambayo anaifanya na mpenzi wake huyo na inatarajiwa kuwa mtaani kesho Jumatano ya Desemba 14, 2016.
Global TV Online ilimtupia swali mpenzi wa Jide ikimuuliza kuwa ni wapi alikutana na mrembo huyo, na haya ndiyo yalikuwa majibu ya Rasta.
“Aaah, i can’t explain it here, but i didn’t meet Jide in Tanzania” akimaanisha kuwa hawezi kuelezea kuhusu mahusiano yake na Jide lakini hakukutana naye hapa Tanzania.
Jide kwa upande wake anasema alikutana na Rasta katika kazi zao za muziki maana wote ni wasanii kama ambavyo wafanyakazi wa benki wanaweza kuingia katika mapenzi kwa kuwa wote wapo karibu kikazi.
Spicy alipoulizwa ni mpango gani anao na dada yetu alisema wanapendana na mambo mengine yatajulikana kadri muda unavyokwenda.
Kuhusu tuzo aliyoipata juzi katika EATV Awards 2016 ya Mwanamuziki Bora wa Kike, Jide alisema amejisikia vizuri na imemtia nguvu katika kazi yake ya muziki.
Global TV Online ilimtupia swali lingine Jide kuhusu mbinu gani aliyotumia kumchunguza mpenzi wake huyo, ambapo alisema hakutumia muda mwingi kumjua na kwamba walipokutana walijikuta wamezama katika mapenzi hivyo haikumchukua muda mrefu kufikiria hilo.
Source; Global publisher
ConversionConversion EmoticonEmoticon