Propellerads

Yanga yawatoa macho wapinzani


Image result for picha za Justine Zulu
KLABU ya Yanga imemsajili kiungo mkabaji wa Zesco United, Justine Zullu kwa mkataba wa miaka miwili.
Mchezaji huyo aliyekuwa nchini kwa siku tatu zilizopita, amesaini mkataba huo jana kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Yanga, ambacho kimepania kufanya vizuri katika ligi na michuano ya kimataifa.
Tovuti ya Yanga iliweka picha za mchezaji huyo akiwa anasaini katika moja ya hoteli kubwa nchini, na kwamba tayari wamemalizana naye kwa mkataba wa miaka miwili.
Gazeti hili lilipomtafuta Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit kuzungumzia usajili huo, simu yake ilikuwa ikiita bila kupokewa. Usajili wake umetokana na mapendekezo ya awali ya aliyekuwa Kocha Mkuu, Hans Pluijm ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi mpya wa benchi la ufundi.
Hadi kukamilika kwa dili hilo, Kocha mpya George Lwandamina anahusika kwa kuwa anamfahamu vizuri mchezaji huyo kwani alikuwa naye Zesco ya Zambia.
Zullu anatarajiwa kuziba nafasi ya Vicent Bossou ambaye hatakuwepo baada ya kudaiwa kupata timu nchini Vietnam.
Mchezaji huyo amecheza Zesco United tangu mwaka 2014 alipojiunga akitokea Kabwe Warriors.
Anatarajiwa kuipa nguvu Yanga kutokana na uzoefu alionayo baada ya kucheza katika klabu tofauti za Afrika, Israel na Ulaya.
Aliwahi kucheza Lamontville Golden Arrows msimu wa mwaka 2012-213, Enosis Neon Paralimni 2012, Hapoel Rishon LeZion 2010 hadi 2012, Hapoel Bnei Lod 2009 hadi 2010, Hapoel Beer Sheva 2007 hadi 2009 na National Assembly 2005 hadi 2007.

Source ;Habarileo
Previous
Next Post »