Propellerads

Muhongo; Umeme kila mahali baada ya miaka mitano



Image result for picha za profesa muhongo


SERIKALI imesema inataka kuondoa tatizo la upatikanaji wa nishati ya umeme nchi mzima ndani ya miaka mitano ijayo. Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau wa nishati endelevu wa nchi zinazoendelea.
Profesa Muhongo alisema katika kipindi hicho cha miaka mitano, serikali imejipanga kuondoa tatizo hilo la umeme kwa kiasi kikubwa ili kuendana na malengo endelevu ya maendeleo.
Alisema katika kufanikisha jambo hilo, bajeti ya wizara hiyo katika mwaka huu wa fedha, asilimia 94 zimeelekezwa katika miradi ya maendeleo, ikiwemo upatikanaji wa umeme wa uhakika.
“Kwa kuzingatia umuhimu wa nishati endelevu nchini, mwaka wa fedha 2016/2017 serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya upatikanaji wa nishati vijijini,” alisema Muhongo na kuongeza bara zima la Afrika linahitaji Sh bilioni 44 kila mwaka hadi kufikia mwaka 2030 kuhakikisha lengo la nishati linakamilika.

Image result for picha za profesa muhongo
Alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi zinatekeleza miradi ya nishati endelevu ili kuhakikisha umeme unapatikana wa uhakika nchi nzima.
“Serikali inataka kuondokana na matatizo ya umeme tuliyonayo sasa ya upatikanaji wa umeme katika kipindi hicho,” alieleza na kuwataka washiriki katika mkutano huo kujikita katika mahitaji ya umeme ili kutekeleza lengo hilo namba saba na kuzitaka sekta binafsi kutoa ushirikiano katika hilo.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez alisema lengo la mkutano huo ni kuangalia ni namna gani nchi zinazoendelea zinaweka mikakati kuweka nishati endelevu ili kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu Namba Saba linalotaka ifikapo mwaka 2030, ziwe na nishati endelevu na kwa bei rahisi.
“Nishati endelevu ni nguzo katika maendeleo ya kiuchumi, jamii na mazingira kama inavyotambuliwa katika ajenda hizo za mwaka 2030 upatikanaji wa nishati ya uhakika kwa wote na kwa bei nafuu," alisema Rodriguez.
Aidha, alisema miaka miwili iliyopita Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) ilikusanya dola za Marekani bilioni mbili kwa ajili ya kusaidia nchi mbalimbali duniani katika miradi ya nishati ambapo zaidi ya nchi 110 ziweze kuendeleza miradi ya nishati endelevu.
Image result for picha za profesa muhongo
“UNDP na washirika wake wanaendelea kusaidia nchi zinazoendelea ili kupatikana uboreshaji wa mitaji ya utekelezaji wa maendeleo na pia kuimarisha taasisi zinazoendesha sekta za nishati,” alibainisha na kuongeza kuwa kutolewa kwa fedha hizo ni kwa ajili ya kufanikisha upatikanaji wa umeme na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Previous
Next Post »