Propellerads

Uwanja wa kisasa kujengwa bagamoyo na wachina..


Image result for picha za jakaya na wachina

MKOA wa Pwani unatarajiwa kuwa na uwanja wa kisasa ambao utasaidia kukuza soka la vijana na kuinua michezo kwenye mkoa huo ambao umepania kuwa moja ya mikoa itakayolea vipaji. Uwanja huo unatarajiwa kujengwa kwenye Kijiji cha Msoga na serikali ya watu wa China, lengo likiwa ni kukuza mchezo huo katika mkoa huo.
Akizungumza katika hafla maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya kwenda kutembelea eneo ambalo litajengwa uwanja huo, Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk Jakaya Kikwete ambae alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo, alisema uwanja huo utajengwa kwa ufadhili wa Serikali ya China.
“Uwanja huu utakuwa mkombozi wa maendeleo ya mchezo wa soka katika mkoa wa Pwani na nchi kwa ujumla. Utasaidia katika kuibua vipaji vya wachezaji chipukizi na kutumika kwenye klabu na timu ya taifa kwa siku za baadae,” alisema Dk Kikwete.
Alisema lengo la ujenzi wa uwanja huo ni kuona kuwa mkoa wa Pwani na Tanzania kwa ujumla inazalisha wachezaji wengi wenye vipaji ambao watatumika kwenye timu ya taifa, klabu mbalimbali na wengine kuuzwa nje ya nchi.
“Nimezungumza na rafiki zetu wa serikali ya China na wamekubali kutujengea uwanja na hilo ni jambo la msingi katika maendeleo ya mchezo wa soka katika taifa letu,” alisema Dk Kikwete.
Image result for picha za uwanja wa mpira
Dk Kikwete alisema kuwa anaipongeza serikali ya china kwa kuona umuhimu wa kusaidia kujenga kiwanja hicho, na kuongeza kuwa pindi kitakapokamilika kitakuwa na michezo mingine ambayo itakuwa ikifanyika mbali na mchezo huo wa soka, lengo likiwa ni kuwapa fursa vijana kuweza kuonyesha vipaji walivyonavyo.
Naye Mwakilishi wa balozi wa China nchini, Yang Tong aliahidi kuendelea kutoa kushirikiana na serikali ya Tanzania hususan katika sekta ya michezo.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete alisema kwamba lengo lake kubwa ni kuhakikisha anakuza michezo katika jimbo lake na kukamilika kwa ujenzi wa uwanja huo kutaweza kuwasaidia vijana kukuza vipaji vyao.

Previous
Next Post »