LONDON, England KILA kona ambayo Arsene Wenger ataikuta, ni lazima atakutana na kikwazo kitakachomzuia achelewe kukamilisha mipango ya muda mrefu aliyojiwekea kwa ajili ya maendeleo ya klabu yake ya Arsenal. Tangu alipoamua kuweka mkakati thabiti na kufanya kila analoliweza kwenye masuala ya usajili ili kufukia gharama zilizotumika kwenye ujenzi wa dimba la Emirates na Arsenal yenyewe kumpa sapoti ya kutosha, tumeona namna timu hiyo ilivyopunguza presha kwa kutopoteza tena mastaa wakubwa ambao kiu yao ilikuwa ni kunyakua mataji na usajili wa Mesut Ozil na Alexis Sanchez mwaka 2013 na 2014...
By Dimba
ConversionConversion EmoticonEmoticon