Propellerads

Vodacom yazawadia wateja wake.....


Image result for picha za vodacom

WATEJA wa kampuni ya simu ya Vodacom wanatarajiwa kunufaika na zawadi za Sh bilioni tano kutokana na promosheni mpya ya “Nogesha Upendo” itakayokuwa na zawadi za fedha taslimu, muda wa bure wa maongezi na MB za intaneti kila siku katika msimu huu wa sikukuu.
Katika promosheni hiyo itakayodumu kwa miezi miwili, zaidi ya wateja 500 wanatarajiwa kujishindia Sh milioni moja kila mmoja katika kipindi chote cha msimu wa promosheni.

Image result for picha za zawadi za vodacom
Akizungumza wakati wa uzinduzi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia, alisema; “Tunayo furaha kuzindua promosheni ya msimu wa sikukuu ya Nogesha Upendo inayolenga kuleta shamrashamra za furaha ya sikukuu kwa wateja wetu."
“Tunajua sikukuu hizi zinaleta familia za kitanzania na marafiki pamoja kufurahi na kutumiana salamu za upendo, tumeleta promosheni hii kwa ajili ya kuwazadia wateja wetu wote kila wanaponunua vifurushi vya muda wa maongezi na data kila siku,” alisema.

Image result for picha za zawadi za vodacom

Previous
Next Post »