Propellerads

Sakata la wamachinga Vs Ma-RC wa mikoa...


Image result for picha za George Simbachawene

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amesema agizo lililotolewa na Rais John Magufuli la kusitisha uhamishaji wa wafanyabiashara ndogo, maarufu machinga, linatumiwa vibaya na wafanyabiashara hao, ambapo sasa wamekuwa wakipanga bidhaa mpaka barabarani.
Kutokana na hilo, Simbachawene amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchini, kuhakikisha wanatafsiri vizuri agizo la Rais ; na si kususia na kuwaacha machinga wafanye biashara zao holela.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hana jana, Simbachawene alisema; “Niwasihi wamachinga watambue haki za watu wengine katika kufanya shughuli zao zikiwemo haki za wafanyabiashara wenye maduka, watembea kwa miguu na wanaotu mia magari na suala zima la utunzaji wa mazingira katika maeneo ya mijini.”
Katika mkutano huo, Simbachawene alisema Desemba 6, mwaka huu Rais Magufuli alisitisha zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara ndogo katika maeneo wanayofanyia biashara zao kwa sasa hadi pale mamlaka husika zitakapoandaa maeneo maalum kwa ajili yao.
“Ingawa maagizo ya Rais yanaonesha anawapenda na kuwathamini wamachinga alipozungumza kwa upendo mkubwa akionesha kuguswa na hali ya maisha ya wamachinga na wananchi wote wasio na shughuli rasmi, lakini wao wanachezea uhuru huo,” alisema.
Aliongeza kuwa pamoja na maelekezo ya Rais, alisisitiza kwamba maagizo yake juu ya wamachinga hayana maana kuwa sasa wafanye biashara zao kwenye barabara za kupita magari na waendesha kwa miguu au kwenye hifadhi za barabara. Msisitizo wa Rais ulikuwa kutengwa kwa maeneo mahususi na hakumaanisha kufanya biashara holela.
“Wakuu wa mikoa na wilaya na mamlaka zote za serikali za mitaa Tanzania Bara na hasa mijini ni kwamba wajipange kutekeleza maagizo hayo kwa ufasaha, weledi na umakini mkubwa ili kuwasaidia wamachinga kufanya biashara zao,” alisema.
Alisema wamachinga wana haki kama wananchi wengine kufanya shughuli zao na kutambua mchango wao kwa uchumi wa taifa.
“Wamachinga watafsiri agizo la Rais kama fursa kwao kwao na Rais anayethamini na kuheshimu mchango wao katika uchumi wa taifa na Rais hakumaanisha wafanye biashara zao mahali popote bila kuzingatia sheria zilizopo zikiwemo sheria za mipango miji na usafi wa mazingira,” alisema.
Alisema wamachinga wawekewe utaratibu wa kupangiwa maeneo ya shughuli zao yenye wateja wa kutosha, miundombinu rafiki na washirikishwe katika michakato yote wakati wa maandalizi hayo, endapo utaratibu mzuri utawekwa na kurasimisha shughuli za wamachinga, wanaweza kuchangia mapato ya halmashauri kwa kiasi kikubwa kuliko utaratibu wa kila kukicha na kufukuzana fukuzana.

Image result for picha za George Simbachawene
Previous
Next Post »